Rais wa Zamani Ufilipino Duterte Rodrigo kuyakabili Mashitaka ya Mauwaji ICC

 




Rodrigo Duterte, Rais wa zamani wa Ufilipino, Amekuwa akihusishwa na uchunguzi na hatua za kisheria katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).


ICC imekuwa ikichunguza kile kinachoitwa “vita dhidi ya dawa za kulevya” (war on drugs) kilichoendeshwa wakati wa utawala wa Duterte (2016–2022). Kampeni hiyo ilikuwa kali sana dhidi ya watu waliotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Duterte anahusishwa na tuhuma kuu za Uhalifu dhidi ya ubinadamu (crimes against humanity, Mauaji ya kiholela (extrajudicial killings) ,Ukatili dhidi ya raia na Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu .

wakati wa kampeni hiyo, Maelfu ya watu waliuawa katika operesheni za polisi au na watu wasiojulikana, Mashirika ya haki za binadamu yanadai idadi inaweza kufikia zaidi ya watu 6,000 hadi zaidi ya 20,000, Wengi walikuwa watuhumiwa wa ngazi za chini, watumiaji au wauzaji wadogo wa dawa

ICC inasema kuna ushahidi wa kuonyesha kuwa, Mauaji hayo yalikuwa sehemu ya sera au mpango wa serikali, huenda yalifanyika kwa utaratibu.
Msimamo wa Duterte na serikali yake
Duterte anakataa tuhuma zote, alisema alikuwa anapambana na uhalifu ili kulinda wananchi Serikali yake ilijitoa ICC mwaka 2019 ili kuepuka uchunguzi, lakini ICC ilisema bado ina mamlaka kwa matukio yaliyotokea kabla ya kujitoa.



Post a Comment

Previous Post Next Post